Picha ya pamoja
BAADHI
ya Wananchi Mkoani Mbeya wamelipongeza Jeshi la Polisi Mkoani hapa kwa
kuendelea kusambaratisha na kumaliza kabisa mtandao wa ujambazi kutokana
na majambazi wengi kukamatwa na wengine kuawa.
Pongezi
hizo zimekuja Siku moja baada ya Jeshi hilo kuwauwa watu watano
wanaosadikiwa kuwa ni majambazi katika majibizano ya kurushiana risasi
kati ya Askari na majambazi hayo katika tukio lililotokea katika kijiji
cha Garijembe Wilaya ya Mbeya.
Katika
kuhakikisha Jeshi hilo linaendelea kufanya kazi katika mazingira
mazuri na kwa mafanikio na kuunga mkono juhudi zao, Wadau mbali mbali
leo wamejitokeza kulichangia jeshi hilo katika Hafla iliyofanyika
katika viwanja vya ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoani hapa.
Hafla
hiyo ambayo mgeni rasmi alikuwa ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na
Usalama ya Mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas
Kandoro Jumla ya Shilingi Milioni 28 zilipatikana vikiwemo vifaa mbali
mbali.
Mwenyekiti
wa kikosi cha Mafanikio cha kuchangisha fedha na michango ya
kuliwezesha Jeshi la Polisi kufanya kazi katika Mazingira mazuri, Julius
Kaijage amesema Askari wa Jeshi la Polisi wanafanya kazi katika
mazingira magumu hivyo ni jukumu la kila mwananchi kuhakikisha
analiwezesha kwa hali na mali.
Katika
Hafla hiyo Jumla ya Pikipiki tano zilinunuliwa ambapo kati ya hizo Tatu
zimetolewa na Benki ya Nmb kwa thamani ya Shilingi Milion 5.4, wakati
kamati ikinunua pikipiki Mbili kwa Thamani ya Shilingi Milioni Moja na
Laki Nane.
|
No comments:
Post a Comment