Injini ya ndege hiyo ikiwaka moto kama ilivyonaswa pichani.
Abiria walijawa na hofu kubwa ya maisha yao baada ya injini ya ndege kulipuka moto ikiwa maelfu ya futi juu ya usawa wa bahari.
Dakika kadhaa baada ya kuruka kutoka uwanja wa ndege mjini Helsinki ikiwa na abiria 168 ndani yake, injini ililipuka na kuwaka moto. Ndege hiyo kutoka Ujerumani aina ya Airbus ilipata matatizo kadhaa ya kiufundi kabla ya kushika moto kutoka kwenye injini yake ya kushoto, dakika 15 baada ya kutoka ardhini. Mlipuko ulitikisa ndege hiyo ya Lufthansa aina ya Airbus A321-200 na mashuhuda waliripoti kusikia kelele za msuguano kabla ya milipuko kadhaa kuvuma kupitia kiunzi cha ndege. Injini ya ndege hiyo ilishindwa kuwasiliana na kukata mawasiliano wakati moto ulipolipuka kwenye ndege hiyo, na kuacha ikiruka kwa kutumia injini moja pekee. Marubani walipambana kuidhibiti ndege hiyo na haraka kugeuza na kurejea Helsinki, kutua kwa dharura dakika 20 tu baada ya kuwa imeruka majira ya Saa 12 jioni ya Jumamosi. Msemaji wa Uwanja wa Ndege wa Helsinki-Vantaa alisema: "Ndege ya Lufthansa ililazimika kutua kwa dharura kwenye Uwanja wa ndege wa Helsinki Jumamosi jioni kufuatia matatizo katika injini ya ndege hiyo." "Ndege hiyo yenye makao yake mjini Frankfurt iliruka kutoka Uwanja wa Helsinki, lakini rubani huyo aliirejesha ndege hiyo Helsinki baada ya takribani saa moja baadaye kufuatia matatizo ya ufundi kugundulika katika injini zake. "Rubani huyo aliutaaribu mnara wa kuongozea ndege kuhusu matatizo hayo yaliyojitokeza kwenye injini hiyo." Ndege hiyo iliweza kutua salama kwenye Uwanja wa Ndege wa Helsinki bila kusababisha majeruhi wowote na abiria hao 162 na wafanyakazi 6 walipelekwa katika hoteli moja. Uchunguzi kamili umeanzishwa na shirika hilo la ndege na kampuni ya Airbus kujua sababu hasa za ajali hiyo. Kampuni hiyo yenye makazi yake Ufaransa, ambayo inazalisha ndege hiyo kubwa duniani ya A380, bado haijathibitisha endapo itasitisha safari zaidi za ndege hizo za A321. source-zero99
No comments:
Post a Comment